Friday, December 31, 2010

BWANA KIKWETE HONGERA!

OMBI LA MSAADA WA LUGHA YA KISWAHILI


(jamaani nisaidieni ku sahihisha na kulainisha lugha ya Kiswahili na nitafurahi mzalendo yoyote akinitumia "posta" nzima hii na masahihisho yake manyanyaphiri@gmail.com, nayeye akiwa Mtanzania, Mkenya, Mrundi, Mrwanda, Mkongo au nchi yeyote ile inayoongea lugha kubwa na takatifu yaKiswahili)


KAULI YANGU



Mtu unavyosoma mambo yanaotokea huko Ivory Coast unaanza kweli kushangaa kwamba hata kama kweli Wazungu walituharibu akili sisi Waafrika, kwani kiwango chenyewe je hakina mwisho?

Kwanini huyo Bwana Gbagbo asimwachie mwenzie Ouatarra angalau awamo moja naye atawale?

Hapana! Mzungu wa Ulaya hayupo katika uchu wa madaraka: bali ni mtu binafsi jinsi alivyoharibika tumboni mwa mama yake au kwenye mbegu zile baba yake jinsi alivyochangia kabla ya kuzaliwa kwake, au nisemeje?

NASI HUKU AFRIKA KUSINI TULIKUWA KARIBU SANA KUPATA MZOZO WA AINA HIYO CHINI YA MADARAKA YA BW. THABO MVUYELWA MBEKI. 

Kusema ukweli, naanza kufikiri..... na naomba msamaha kwa wote wanasiasa waliozaliwa 21 May hadi 21 June... nafikiri inahusiana na jinsi Mapacha/Gemini walivyokuwa.  Unaambiwa, hata akiwa mpumbavu, kila mara Pacha anavyotoa kauli utaapa hamna mtu mwenye akili kumshinda yeye: yaani wana kipaji hicho lakini kipaji chenyewe kinagewuka kuwa balaa kwa akina Thabo Mbeki na Laurent Gbago. Vilevile nimeangalia video zake pitia YOUTUBE jinsi anavyo chezacheza ngoma kuwaburudhisha (kuwapumbaza?) wananchi wa Ivory Coast (nilitaka kusema "bwege" lakini sistahili kwani yule ndugu bado ni raisi wa nchi, au raisi-nusu wa nchi mpaka sasa hivi)



 Ni wakati kama huo ambapo mie hukaa na kuthamini vilevile na kushukura Tanzania na watu wake, kwani kulifika wakati ambapo Bw. Julius Kambarage Nyerere mwenyewe alitamkia dunia:"Nang'atuka".

Alikuwa amewiva sana kwa kisiasa nasi Waafrika Kusini (hasaa wanasiaa waliyowahi kupigania uhuru) tulijifunza mengi kwake, chambacho kilitusaidia sana kumtoa madarakani Bw. Mbeki pale alipoaanza kujifanya "president-of-the-republic-of-south-africa-for-life".


Kifupi naandika "posta" yangu ya kwanza kwenye "blog" ya kwanza kwa lugha ya Kiswahili  kukupa wewe Mheshimiwa Raisi WaJamhuri Yamuungano WaTanzinia, Bw. Jakaya Mrsiho Kikwete kuwa kiongozi wa nchi shwari kuliko zote Barani Afrika. Mie binafsi najigamba sana kwa kwelimishwa na WaTanzania (Chuo Cha Waandishi WaHabari Tanzani, Ilala, Dar es-Salaam).

Vilevile najigamba sana kuwa ninao ndugu wa damu kabisa ambao ni Watanzania, Wakenya, Warundi, vilevile na Waganda (sisi ni damu moja tu na Mzungu asije kutubabaisha kwa ukolini-mamboleo).

Ndoto yangu ni kwamba sitakwenda kaburini kabla hatujavunja hii mipaka waliyotengeneza Wakoloni kutugawa angalau toka Afrika Kusini hadi Kenya!







Bwana Kikwete, Mheshimiwa!

Miezi chache iliyopita uliwahi kupata (pitia uBalozi waTanzania Afrika Kusini) jumla ya DVD nane (8) kuhusu mke na watoto wa Mwafrika Kusini waliyo bakizwa na kuterekezwa Tanzania kutokona na ukabila wa hilo kabila-tawala laAfrika Kusini: kabila anakotokea Bw. Nelson Rolihlahla Mandela.

Mimi basi ndie aliendaa na kutuma hizo DVD ambacho zimepokelewa pia na Mfalme Mswati III Nchi Swaziland, Bw. Robert Gabriel Mugabe wa Zimbabwe, Bw. Jacob Gedleyihlekisa Zuma wa Afrika Kusini vilevile na wenginevyo hasa nchini humo.

Barua iliyoambatana na DVD hizo ilikuwa tu ni ombi kwa Raisi Zuma anisaidie kuleta mke na watoto wangu toka Tanzania kwani swala lao ni ukabila-kinaganaga tu kutoka kwandugu zake Bw. Nelson Mandela: hata Tume ya Mapatanisho (Truth and Reconciliation Commission) nchini humo iligundua hivyohivyo ingawaje ilishindwa kusema wahusika (Major General Daniel Mohato Mofokeng na wenginevyo mmoja wao Bw. Benson Mandindi aliyechinjwa hapo baadaye kama kuku barabarani Pretoria kwa makosa mengine yasiyohusiana na Phiri) wapelekwe mahakamani, kwani enzi hizo raisi wa nchi alikuwa huyohuyo Mandela anayejifanya baba wa ANC na Taifa kwa kumwibia mwanzilishi wa chama cha ANC, Bw. Pixley Isaka kaSeme ambaye, inavyoelekea, Bw. Nyerere alikitaja kijiji kimoja kaskazini ya Tanzania kumkumbuka yeye.


Cha kuhuzunisha, Bwana Raisi Watanzania, ni kwamba huyo Raisi wetu Zuma, hadi leo hii, hajafanya lolote kunisaidia mimi Goodman Manyanya Phiri.

Wachambuzi wasema, Bw. Mandela na kabila lake (hasaa huyo Bibi Lindiwe Nonceba Sisulu aliyopewa Wizara ya Ulinzi ambamo mie nafanyia kazi na kuwindwa kwa mashtaka ya uongo kusudi nifukuzwe) walichangia sana kumwepusha Bw. Zuma kwenye hanga la kutoswa jela kwa shtaka la wizi wa hela za serikali.


Kutokana na hayo, wachambuzi wanafafanua zaidi, Zuma anadeni kubwa kwa hao wabaguzi wakikabila kiasi kwamba hayupo tayari kusaidia mtu anayelalamika kwa ukandamizi wa kabila la Bw Mandela , ukandamizi wanaoufanya kwa kusaidiana na Wazungu, hasa Waingereza wa Afrika Kusini wakisaidiana na Waingereza wa Ulaya aliyewaalika Mandela hasa jeshini kuhusika kwa mambo karibu yote!


Kwa kumaliza, ningekuomba sana, Mheshimiwa Bw. Raisi Kikwete, ujipe muda tafadhali wa kwongea naye Raisi wetu Zuma na kumkumbusha kwamba madaraka ya uraisi, kama Bara letu lilivyofunzwa na Tanzania, sisehemu tu ya kujifurahisha kwa mtu binafsi au kujiepusha katika ka mashtaka ya wizi wa hela, bali ni sehemu ya kusaidia wananchi wote bila woga wala upendeleo.  La sivyo Afrika Kusini nayo inaelekea katika lilelile janga ambamo Ivory Coast ilimo.

Hayo yakitokea, basi, kazi zote na jasho lote Wananchi waTanzania waliyotoa kuwasaidia Waafrika-Kusini itakuwa bure tu.


Tusaidie, Bw Kikwete. Wewe ndio nguzo ya Afrika sasa, amini usiamini! HONGERA SANA KWA KUCHAGULIWA TENA KAMA RAISI WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA!


Nashukuru sana. Na, pia kwa kurudia, kumradhi sana kwa Kiswahili uchwara! (Najifunza bado!)


12 comments:

  1. Hodi hapa sioni kama kiswahili chako kimepinda. HONGERA.

    ReplyDelete
  2. ndugu yangu kiswahili chako hakina mushkeli. hongera kwa kiswahili chako kizuri

    ReplyDelete
  3. Ndugu zangu NaNgonyani, John Mwaipopo nawe Chib!

    Ngoja niwashukuru sana kwa kunipa moyo. Mungu awabariki sana; na kwa wale kati yenu wasiyemwamini Mungu, mupate baraka kwavyovyote vile...maana yake ardhi hii ni yetu sote!

    ReplyDelete
  4. Naam!! Nami nabisha hodi hapa.
    WaSwahili husema MFICHA UCHI HAZAI. Na kama kuzaa kiSwahili bora ni kukiandika vema, basi hutaweza kuandika na kukosoa kama huandiki ukakosolewa.
    Kama nisemavyo kila siku, hizi BLOGU NI SHULE. TUNAFUNZA HUKU TUKIFUNZWA.
    Naamini kwa kuingia hapa nitajifunza mengi kutoka nchi ambayo sijawahi kuitembelea.
    Ni faraja saana kusoma lugha hii toka upande wa pili wa dunia
    NIMEFURAHI KUFIKA HAPA, NA SASA NINAHAMIA
    Baraka kwako Bwn Phiri

    ReplyDelete
  5. Nami naomba nijitambulishe hapa. Mimi ni mwalimu wa Kiswahili. Ni "mtaalamu" pia wa mambo ya isimu (Linguistics). Napenda nichukue nafasi hii kukuhongeresha kwa jinsi unavyoimudu lugha hii. Kama wengine waliotangulia, na mimi nategemea kujifunza mengi hapa kibarazani kwako.

    Nimekuwa nikiulizwa na wanafunzi wangu wengi hapa Marekani eti ni kwa nini Afrika Kusini - taifa lenye nguvu, uchumi imara na utajiri mkubwa wa kiuchumi - waafrika wengi weusi bado ni masikini? Pia kuna mwandishi mmoja kutoka huko alikuja hapa kutoa mhadhara. Yeye alisema kwamba weusi wa Afrika Kusini wamezidi na bado wanazidi kusikinika. Eti ni afadhali hata wakati ule wa makaburu. Sijui kama hii ni kweli. Nategemea kwamba nitapata fununu kuhusu jambo hili kupitia blogu hii.

    ReplyDelete
  6. Kazi nzuri mkuu, unajua kwanini wanablog tunaitana wakuu, tunamaanisha kuwa sote tupo vitani na mwenzako ni `mkuu' wako, yaani `afande'...or in english `sir'!
    Hongera sana, kiswahili chako kipo safi, na usiogope kabisa kuandika, kwa kuzania kuwa `unaandika kiswahili sio sanifu' sisi wenyewe ukichunguza tunavyoandika kwenye blog zetu tunaandikiwa kiitwacho `kiswa-english'
    TUPO PAMOJA MKUU,
    Nimefurahishwa sana na haya maneno:
    `Ndoto yangu ni kwamba sitakwenda kaburini kabla hatujavunja hii mipaka waliyotengeneza Wakoloni kutugawa angalau toka Afrika Kusini hadi Kenya!'
    Kikwazo kikubwa cha kufikia ndoto hii ni `viongozi', kwasababu wanaogopa kunyang'anywa viti vyao...lakini sisi kama wananchi wa kawaida tutaungana kwa kutembeleana, na kujuana, kama hivi sasa tumekuwa wandugu wa blog, kiasi kwamba mmoja asipoonekana hewani kwa muda tunaulizana kulikoni!
    Nashukuru tena na HONGERA SANA KWA KUKIPENDA KISWAHILI

    ReplyDelete
  7. @miriam3

    Umenishtua sana pamoja na maneno mazuri ya pongezi. Kumbe nilikuwa nimezubaa kwamba POSTI yii inamaoni mengi kiasi hiki? Niombe basi kumradhi kwawasomaji wote na wale waliotoa maoni yao pamoja na kujitambulisha... kwanza mimi mwenyewe nijitambulishe kwani mie bado mchanga katika mambo haya ya blogging... sisi kwetu Afrika Kusini kutokana na mfumo wa Apartheid uliyemnyima mswahili hapa elimu halisi, hatuko kama nyinyi Watanzania, Wakenya, Warundi na kadhalika kielimu: tunajifunza tu KWENU WALA MUSIAIBIKE KWAKUTOA MAFUNZO KWA WATU SISI WENYE MIJI YENYEMAGOROFA MAREFU NA MIBARABARA PANA BURE, ILA MTUONEE HURUMA JAMAANI KWA ELIMU YETU YA KIWANGO CHA CHINI!!!.


    Nitapata muda baada ya kurudi BANKI kujaribu kusoma maoni yote na kuwakaribisha moja moja wote wale waliotoa michango hapa. Vilevile muda nitatumia kujiunga na blogi za wote nyie WAKUU zangu Dada Miriam na wenginevyo waliojitambulisha hapa.


    "KIONGOZI ASIYETAMBUA KWAMBA KAMPYUTA NDIO INATAWALA ULIMWENGUNI SASA HIVI BASI AMEKWENDA NAMAJI... ANGALIA TUNISIA, MISRI ETC." ndio ujumbe wangu kwa sasa hivi Mkuu Miriam kwamba "tutafika tu umojani Wa Afrika!"

    Mungu Ibariki Afrika!

    ReplyDelete
  8. This comment has been removed by the author.

    ReplyDelete
  9. Karibu bwana Manyanya Phiri. tunahitaji michango ya mawazo toka kwa wanaharakati kama wewe kwa lengo mahususi la kuielimisha jamii ili tuweze kuondokana na umasikini unasababishwa na utawala mbovu wa viongozi wengi katika bara letu la Afrika.

    ReplyDelete
  10. Phiri: Sahihisho kidogo, ni kwamba Miram3 ni mwanaume. Japo wewe si mtu wa kwanza kumwita dada Miriam, Miram3 changamoto unayo kuondoa huu utata unaojitokeza mara kwa mara kukutambua kama wewe ni Adam au Hawa. Kazi kwako Miram3!

    ReplyDelete
  11. LOL! (Na asante kwa sahihisho Malkiory, Mkuu!)


    Asante pia kwa kujiunga na blogu yangu ya msingi ambayo ni Barua kwa Bw Jacob Zuma kwa lugha ya Kiingereza (http://goodmanmanyanyaphiri.blogspot.com)


    Labda ndugu yetu Miram3 ana undugu na Mengistu Haile MARIAM (http://www.independent.co.uk/news/world/africa/former-ethiopian-dictator-mengistu-sentenced-to-death-834594.html)

    Tumpe labda nafasi zaidi atutambulishe yeye kwetu jamaani!


    ....KAMA AKITAKA, LAKINI!

    ...Maana yake, miaka 131 iliyepita huko Wingereza alikwepo mwandishi maarufu sana mwenye jina la George Eliot [http://en.wikipedia.org/wiki/George_Eliot] na asingekuwa anatumia hilo jina-dume huyo mwana-mama hamna hata kitabu chake kimoja kingechapishwa kwani wanawake walikuwa wanadharaurika sana enzi hizo huko Uingereza!

    Na leo mimi Rafiki yangu Malkiory umenitoa mvutio kidogo kujuwa kwamba kumbe yule siyo mwanamama (LOL!)


    Sisi sote ni binadamu lakini, ukiwa mwanamke au mwanaume HATA UKIWA KATIKATI dunia nawe ni yako tu!

    Vilevile mtandaoni hapa tunaheshimu mawazo yako tu siyo kingine naye yule ana akili sana. Je umeona toleo lake mpya: "MPENDE JIRANI YAKO-1 (http://miram3.blogspot.com/2011/03/mpende-jirani-yako-1.html)"?

    Moto wa kwotea mbali nakwambia!!!! Nakushauri tembelea huko, Malkiory Rafiki yangu ufaidi!!!

    Lakini asante sana tena kwa kunikaribisha kati ka jumuiya ya wanablogu wa Kiswahili: nitajitahidi kusahihisha zaidi pia Kiswahili changu mtandaoni!

    ReplyDelete