Monday, January 31, 2011

YESU PEKE YAKE AFRIKA KUSINI

Nchini mwetu Afrika Kusini ni Yesu peke yake (labda pamoja tu na ndugu Zake na wafuwasi) anayeruhusiwa kushughulika na mipango ya taifa hili la kiKrestu.  Wale wanaomwamini Shetani ni lazima kila pengo lizibwe wasije wakapata mwanya nao wakung’aa kama Yesu waMji WaQunu huko Cape Mashariki badala ya Yesu waMji Nazareth.


Nipe muda basi nifafanue zaidi kabla ya mwisho ya wiki hii, lakini ukitaka kusoma maoni yangu kwa lugha ya Kiingereza, bonyeza hapa. Nawale pia wanaojiamini katika lugha ya Kienjeji tena yapili Bararani Afrika (Kizulu) wanaweza kubonyeza hapa

15 comments:

  1. Mkuu naripoti tu nipo sana kambi hii kwa hiyo kama hujastukia nikisema kitu jua bado nafyonza karibu vyote uandikavyo KINGEREZA na KISWAHILI !

    Hivi Mkuu GOODMAN unazungumza lugha ngapi tukiachilia zile uwezazo kuziandika?

    ReplyDelete
  2. Swali la Kaka Kitururu ni jema.
    Labda mimi niongeze kuwa UNASIKIA na KUELEWA lugha ngapi mbali na zile unazoandika na kuongea?
    Hahahahaaaaaaaaaaaaaaa
    Siku njema Kaka

    ReplyDelete
  3. Mtakatifu na Mzee wa Changamoto: Swali zuri.

    Kuna wakati nilijifunza Kizulu ingawa sasa nimeshasahau kila kitu. Kuna mtu mkutanoni alishangazwa na majina yangu - masangu matondo, nikawa mdadisi mpaka nikaanza kujifunza lakini hizo "clicks" baadaye zikanishinda. Natamani kama ningeendelea!

    ReplyDelete
  4. jana nilikutana na jamaa mmoja hapa mbeya anaongea lugha za sehemu zote alizokaa tanzania. yeye ni mnyakyusa lakini anaongea kisafwa, kisukuma, kihaya, kikurya na kikerewe.

    Goodman (mtu mwema) nataka kujifunza kizulu. nianzie wapi?

    ReplyDelete
  5. Ndugu Watanzania!

    Ndugu nyote wanaochangia hapa kutoka nchi mbalimbali zinazoongea lugha kuu yetu yaKiswahili.


    Wasomaji wa Blogi yangu mpya


    Nanyinyi nyote Waafrika wenzangu wakiwa Wakizungu, Wakiswahili na makabila mengine kutoka Cape Town hadi Cairo


    Binadamu wenzangu wasomaji wa Blogi yangu kote duniani


    Nasema tu ASANTENI SANA kwa kuniunga mkono. Ingawaje tarehe 4 mwezi wa tano
    ???natihimiza??? (“I COMPLETE”) umri wa miaka 50, mimi bado ni mtoto mchanga katika mambo haya BLOGGING.


    Nitahitaji daima kupata msaada na kuungwa mkono nanyinyi hapo, tafadhalini.


    Kwako Bwana Masangu Matondo Nzuzullima (MMN), Mkuu! Nawe John Mwaipopo, Mkuu!


    Kama mnataka (niFUNA) kuimarisha (UKUJULISA) Kizulu chenu, basi Mungu akijalia nitakuwa natoa masomo (IZIFUNDO) ya misingi ya Kizulu hapahapa.


    Kwa taarifa yenu, Wakuu: Kizulu, Kiswahili,, Kindebele, KiXhosa, Kiswati (cha huko Swaziland na hapa Afrika Kusini) vimekaribiana ya kutosha kumfanya mtu mwenye misingi ya lugha moja asishindwe kwelewa lugha yingine.


    Mimi naamini isingekuwa kwamba Wakoloni walitaka kutugawa ili watutawale, lugha zote hizi zingeitwa lugha moja (mfano “Kingoni”) na hizi zote zinginezyo zijulikane kama DIALECTS tu badala ya lugha zenye kujitegemea.


    Kuhusu swali: “lugha ngapi naongea?”


    Kwako Bwana Kitururu na Mzee wa Changamoto (lazima niwe mfuasi wa blog yako Mzee wa Changamoto lakini kama unayo kwanza blogi yakwako binafsi), mie naongea na kwandika angalau kwa jitihada:


    1. Kiswahili, Kiingereza, Afrikaans, Xhosa, Swazi, Zulu

    2. Nao wale wanawoongea KiChewa, KiTumbuka (zote za Malawi anakotokea baba yangu mzazi) Kireno na lugha zifwatao za huku Afrika Kusini, Msumbiji, Lesotho na Botswana: KiSotho, Kipedi, Kitswana, KiTsonga.

    Lugha ambayo bado sijayielewa kabisa ni lugha moja ya Afrika Kusini kaskazini (karibu na Zimbabwe). Nayo inaitwa Kivenda.


    Kama ningeorodhesha lugha ninazoongea kwa kujiamini ningesema 1. Kizulu (isiZulu) 2. Kiingereza 3. KiSwati (Siswati)4. Kiswahili na kadhalika!


    Kwakumnukuu Ndugu John Mwaipopo:
    ‘Jana nilikutana na jamaa mmoja hapa Mbeya anaongea lugha za sehemu zote alizokaa Tanzania. Yeye ni Mnyakyusa lakini anaongea Kisafwa, Kisukuma, Kihaya, Kikurya na Kikerewe.’


    Sasa pendekezo, jamaani: Mnaonaje tuanze blogi (“LINGUAFRIKA”/ “NDIMIBLOG”/ETC) yakuchangia pamoja (Tuwe editors watu watano au zaidi) na kila mmoja wetu awe “mtaalam” wa lugha moja mfano Kiswahili kwa Bibi X, Kindengereko kwa Bwana Y, Kizulu kwa Bwana Phiri, Kifransa kwa Bwana Z na kadhalika? Tuwe kama tunatengeneza DICTIONARY, THESAURUS au kitu kama hicho ili tusaidie ???vizazi???(GENERATIONS) ???vijazo/vijao kuwa na lugha moja yasisi Waafrika.
    Sijui hapo kama nimebwata tu; lakini nimetoa wazo na pendekezo kama lilivyonifikia kichwani wakati nilipokuwa naandika hapa.



    Asanteni tena!

    (P.S. Kwako Yasinta Ngonyani, Mkuu! Sina la kusema zaidi kwamba nilianza kujua Blogi za Kiswahili pitia blogi yako. Mungu akubariki daima!)

    ReplyDelete
  6. @Goodman : Asante Mkuu! Kwangu wewe ni baadhi ya watu naoamini wananielewa hata pale kwenye kijiwe changu hata wakati kuna waonao ni UJINGA tu niandikao na LUGHA chafu!


    Na kwenye Blogu zako nimepata picha na elimu tofauti ambayo najivunia!
    Na kwa kuwa upo najua kuna mwalimu mwingine nimepata nikikwama naye wa kumuuliza!

    Ni hilo tu MKUU!

    ReplyDelete
  7. Kuna baadhi ya watu wana vipaji vya kushika kwa haraka lugha mbalimbali hata kama zinatofautiana sana. Mimi ni jamaa yangu anaongea kiingereza, kiswahili, kichina, kijerumani, kispaniola, na lugha za nyumbani ndio usiseme, za ukanda wa ziwa anaongea zote, kikinga na kinyakyusa pia.

    ReplyDelete
  8. Tupo pamoja mkuu, nilikwazwa kidogo na mabomu ya Gongolamboto., nashukuru nipoo salama. Hongera sana kwa kujua lugha mbalimbali hasa za bara letu la Afrika, wewe ni `mzalendo halisi wa Afrika, HONGERA SANA

    ReplyDelete
  9. @chib. Nafikiri siri kubwa ya kujua lugha ni kuwapenda binadamu wenzio. Wako WaSouth-Afrika waliokaa zaidi ya miaka 10 Tanzania lakini hadi leo hii hawajui lolote kuhusu Kiswahili. Kwa wakati wote ule WALIJITENGA!!!!


    @Mam3. “Gongo la Mboto” nasemaga: “Usiguse! Poleni sana!” Kwani wewe Mkuu unaishi maeneo hayo?

    Binafsi, ninaye Mdogo wangu (mtoto wa amu au baba-mdogo) anayeishi eneo hilohilo karibu na uwanja wandege. Hadi leo nimeshindwa kuwasiliana naye ili kumwuliza hali. Poleni tena!


    @Kitururu. Mkuu, hapo umenimaliza. Mimi simtu, Bwana! Hata huku kwetu watawala wanataka kunifunga kutokana na msimamo wangu dhidhi ya ukabila wa hilo kabila la Bwana Nelson
    Rolihlahla Mandela. Sasa sifa kama hiyo unayonipa yanimaliza kabisa! Mimi nakuombea wewe hapo maisha marefu tena ya uwezo zaidi ya kuchimba zaidi maana yake kuwa Mwafrika

    ReplyDelete
  10. Bwana Phiri: Kule katika blogu yangu uliwahi kuacha maoni kwamba ulikuwa na wasiwasi na Kiswahili chako.

    Usiwe na shaka. Kiswahili chako wala hakina tatizo lolote. Endelea kutuelimisha na kutuletea mambo ya huko Afrika Kusini.

    ReplyDelete
  11. duhu hii kali ya lugha elfa, unanena kwa lugha. mimi najaribu kuongea lugha kadhaa ila nyingi kwa mtizamo wa kikoloni ni ushenzi

    nazungumza kihaya, kinyankole, kiganda, kinyambo, kiswahili na kiingereza.

    nasikia kinyarwanda, kinyangara, kikurya na sasa nataka jua kuzulu achilia mbali ki-Xhosa

    ReplyDelete
  12. Kizulu siyo kigumu kabisa. Ni hatua moja tu kutoka Kiswahili hadi Kizulu. Na kule kutoka katika Kizulu kwenda Kixhosa, Kindebele na Kiswati nisawasawa na kutoka kidole kimoja kwenda kingine tu.

    Mimi napendekeza tuanze blogu pamoja nawe na wengineo Barani na kila siku tutowe neno moja (WORD OF THE DAY) na hilo neno tuzungumzie kwalugha kadri tunavyokuwa nao wahariri wa lugha hizo tunaoshirikiana nao pamoja juu ya hiyo blogu.

    Kwasasa hivi, mpaka hapo tutakapopata wataalamu wenye ujuzi zaidi yetu,

    Wewe Mkuu uwe EDITOR waKihaya, Kinyankole, Kiganda, na Kinyambo;

    Nami Manyanya niwe EDITOR wa Kiswati (Swaziland na South Africa), Kizulu labda na Kixhosa mpaka hapo tutakapopata wengine wa kutusaidia.


    Mfano: WORD OF THE DAY: "PERSON" or "A PERSON"

    Swahili: "mTU", plural: "waTU"
    Zulu: "umNTU", plural: "abaNTU"
    Swazi: "mNTFU", plural: "baNTFU"
    Kihaya: "...", plural: "...."
    Kinyankole: "....", plural: "..."
    Kiganda: "....", plural: "..."
    Kinyambo: "....", plural: "..."





    Kama wazo langu unalipenda nitumie basi email kusudi blogu hiyo nianzishe na kukutumia PASSWORDS zake kusudi wote wawili (na wengineo wapendao wazo hili) tushirikiane kuiandika. Email yangu manyanyaphiri@gmail.com

    ReplyDelete